Addis Ababa,Ethiopia.
Kilimanjaro Stars imetinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Cecafa Chalenji Cup baada ya leo jioni kuibanjua Rwanda kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali wa kundi A uliopigwa katika dimba la Addis Abba.
Magoli ya Kilimanjaro Stars yamefungwa na Said Ndemla dakika ya 22 kwa mpira wa adhabu huku lile la pili likifungwa na Simon Msuva dakika ya 75.Goli la kufutia machozi la Rwanda limefungwa na Jacques
Tuyisenge dakika ya 85.
Kufuatia matokeo hayo Kilimanjaro Stars imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ikiwa imejikusanyia pointi sita baada ya kushuka dimbani mara mbili.
Katika mchezo wa mapema uliopigwa saa 8:00 mchana Zanzibar Heroes ilikubali kichapo cha mabao 4-0 toka kwa Uganda na kupoteza matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali.
Magoli ya Uganda Cranes yamefungwa na Farouk Miya aliyefunga mara mbili, Erisa Ssekisambu na Ceaser Okhuti.Zanzibar ilipata pigo baada ya nyota wake wawili Mwadini Ally Mwadini na Yahya Mudathir kulimwa kadi nyekundu.
Siku ya Jumatano, Malawi itamenyana na Djibouti huku Sudan Kusini ikicheza na jirani yake Sudan.
Mchuano mwingine Somalia watamenyana na Ethiopia huku mabingwa watetezi Kenya wakimenyana na Burundi.
0 comments:
Post a Comment