Torino,Italia.
Mlinda mlango nguli wa Italia Gianluigi Buffon anaamini kuwa Iker Casillas ndiye mlinda mlango bora zaidi wa zama zake na kudai kuwa Petr Cech ndiye mlinda mlango aliyekamilika zaidi katika kipindi cha miaka mitatu ya hivi karibuni.
Akiongea na gazeti la Marca la Hispania,Buffon,37 ambaye wiki iliyopita alitimiza miaka 20 tangu aanze soka la ushindani amesema
“Mlinda mlango bora wa zama zangu ni Casillas.“Amekuwa bora sana katika mikono yake.
“Watu wanataja majina kama [Lev] Yashin, [Ricardo] Zamora, [Dino] Zoff, [Sepp] Maier na [Gordon] Banks.
“Kama ningeambiwa nichague walinda mlango bora wa zama zangu,basi ningesema [Peter] Schmeichel, [Walter] Zenga, [Gianluca] Pagliuca, [Andoni] Zubizzareta.
“Lakini katika muongo uliopita Cech na Casillas wamekuwa bora sana.Katika miaka hii mitatu ya karibuni ningesema [Manuel] Neuer,kwani amekuwa bora sana hasa katika kucheza mipira ya juu.
0 comments:
Post a Comment