Manchester, England.
Manchester United imelazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ngumu ya Leceister City katika mchezo mkali wa ligi kuu uliopigwa usiku wa leo katika dimba la King Power.
Manchester United ambayo iliingia katika mchezo wa leo kusaka pointi tatu muhimu ili ikae kileleni ilijikuta nyuma dakika ya 24 baada ya Jamie Vardy kufunga goli akimalizia kazi nzuri ya Christian Fuchs.
Kuingia kwa bao hilo kuliifanya Manchester United iamke na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 45 kupitia kwa kiungo wake Bastian Schweinsteiger aliyefungwa kwa kichwa akiunganisha kona ya Juan Mata.
Kufuatia sare hiyo Manchester United na Leceister City zimeipisha kileleni Manchester City ambayo imefikisha pointi 29 baada ya kuifunga Southampton kwa mabao 3-1 katika mchezo wa mapema uliopigwa Etihad.
Rekodi yawekwa!!
Jamie Vardy aweka rekodi mpya baada ya goli alilofunga dhidi ya Manchester United leo kuwa ni la 11 katika michezo 11 mfululizo akiivunja rekodi ya mwaka 2003 ya Ruud Van Nistelrooy ya kufunga magoli 10 katika michezo 10 ya ligi kuu.
Vikosi
Leicester City: (4-4-2) Schmeichel;Simpson (De Laet, 80), Morgan, Huth,
Fuchs; Mahrez, Kanté, Drinkwater,Albrighton (Schlupp, 70); Okazaki (Ulloa,
60), Vardy.
0 comments:
Post a Comment