London,England.
Arsenal imepata pigo baada ya kiungo wake mkabaji Francis Coquelin kuripotiwa kuwa atakuwa nje kwa kipindi cha kati ya miezi mitatu au minne baada ya kuumia goti lake la mguu wa kulia.
Coquelin,24 alipata jeraha hilo siku ya jumamosi baada ya kugongana na kiungo wa West Bromwich Albion Claudio Jacob wakati wakigombea mpira katika mchezo ambao Arsenal ililala kwa mabao 2-1 na kushindwa kukaa kileleni mwa ligi kuu ya EPL.
0 comments:
Post a Comment