London,England.
ARSENAL imeanza mchakato wa kuziba pengo la kiungo wake aliye majeruhi Francis Coquelin baada ya kuripotiwa kumuita kwa majaribio kiungo asiye na timu Mghana Ismail Abdul Razak.
Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali zilizoibuka siku ya jumapili na kuripotiwa na Metro ni kwamba Ismail Abdul Razak,26 mapema wiki iliyopita alikubaliana na Arsenal juu ya kufanyiwa majaribio hapo mwezi Desemba na akionyesha kiwango kizuri atasajiliwa moja kwa moja.
Je Razak ni nani???
Ismail Abdul Razak:Alianza safari yake ya soka kwa kuichezea klabu ya Hapoel Acre ya Israel kabla ya kuichezea Real Valladolid ya Hispania kwa miaka mitatu kisha kutupiwa virago.
Nafasi uwanjani
Razak hucheza kiungo au ulinzi wa kati
0 comments:
Post a Comment