728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, November 16, 2015

    RONALDO:KWA KOCHA HUYU HATUWEZI KUSHINDA TAJI LOLOTE LA MAANA

    Madrid,Hispania.



    Mahusiano kati ya Cristiano Ronaldo na kocha Rafael Benitez yameendelea kuwa mabaya baada ya nyota huyo kumwambia Rais wa klabu hiyo Florentino Perez kuwa Real Madrid isitarajie ubingwa wowote wa maana msimu huu ikiwa chini ya Benitez.

    Ronaldo,30 ameripotiwa na gazeti la El Confidential la Hispania kuwa alitoa kauli hiyo wiki iliyopita baada ya Real Madrid kubamizwa mabao 3-0 na Sevilla katika muendelezo wa michezo ya ligi ya La Liga.
    Rafael Benitez and Cristiano Ronaldo

                                                                  Benitez

    Hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kuwepo kwa mgogoro wa chini chini kati ya wawili hao (Ronaldo na Benitez) hali iliyoripotiwa kuanza kuivuruga klabu.Ronaldo anadaiwa kutofurahishwa na soka linalofundishwa na kocha huyo ambalo linataka timu nzima iwe na jukumu la kujilinda hali ambayo anaiona kuwa inamnyima nafasi za kufunga magoli ya kutosha.

    Wakati huohuo Ronaldo pia ameripotiwa kuwa katika msuguano mwingine na Rais wa klabu hiyo Perez kwa madai kuwa Perez yuko karibu zaidi na Gareth Bale kuliko yeye Ronaldo.Ronaldo amejikuta katika hali hiyo kufuatia habari kuenea kuwa Perez amechukizwa na nyota huyo Mreno kila mara kusema ataondoka Real Madrid.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RONALDO:KWA KOCHA HUYU HATUWEZI KUSHINDA TAJI LOLOTE LA MAANA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top