728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, November 16, 2015

    KIBADENI AITA NYOTA 21 KILIMANJARO STARS TAYARI KWA MICHUANO YA CHALENJI

    Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’, Abdallah Kibadeni
    ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kujiandaa na michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza kutimua vumbi Jumamosi Novemba 21, nchini Ethiopia.

    Kibadeni anayesaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda, amesema wachezaji aliowaita wapo katika hali nzuri na wamekua wakifanya
    mazoezi na kikosi cha Taifa Stars ambapo wao kama benchi la ufundi wamepata nafasi ya kuwa nao kwa muda mrefu na kutambua maendeleo yao.

    “Tumechagua wachezaji kulingana na mahitaji ya timu, tumekua na wachezaji hawa kwa muda mrefu katika vipindi mbalimbali, tunaamini tuliowachagua watafanya vizuri katika michuano hiyo mikongwe barani Afrika”
    amesema Kibadeni.

    Wachezaji walioitwa ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam),Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi
    Shomari Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa),
    Juma Abdul (Yanga) na Kelvin Yondani (Yanga).

    Viungo Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Said Ndemla (Simba), Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Deus
    Kaseke (Yanga).

    Washambuliaji John Bocco
    (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga) na Saimon Msuva (Yanga).

    Michuano ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21 na kumalizika Disemba 6, ambapo Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A, lenye wenyeji Ethiopia, Rwanda na Somalia.

    Wachezaji Said Mohamed, Juma Abdul,Hassan Kessy, Hassan Isihaka, Salum
    Abubakar na Ibrahim wanaendelea na mazoezi
    jijini Dar es salaam chini ya kocha msaidizi Juma Mgunda wakati wanawasubiri wachezaji wengine walioko nchini Algeria na kikosi cha
    Taifa Stars.

    Kundi B lina Bingwa Mtetezi Kenya, Burundi,Uganda na Zanzibar, huku kundi C likiundwa na timu za Sudan, Sudani Kusini, Djibouti na
    waalikwa wa michuano hiyo timu ya taifa kutoka Malawi.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KIBADENI AITA NYOTA 21 KILIMANJARO STARS TAYARI KWA MICHUANO YA CHALENJI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top