Cole:Manchester United inataka kumpa mkataba wa muda mfupi mlinzi wa zamani wa vilabu vya Chelsea na Arsenal Ashley Cole,35 ili kuziba nafasi ya mlinzi wake majeruhi Luke Shaw.(The Sun on Sunday)
Pato:Tottenham itamgeukia mshambuliaji wa Corinthians Alexandre Pato kama itashindwa vita ya kumsajili mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino ambaye pia anawindwa na vilabu vya Chelsea na Manchester United.(Daily Star)
Ronaldo:Kocha wa Manchester United Mdachi Louis van Gaal amekiri kuwa anataka kumsajili nyota wa zamani wa klabu hiyo Mreno Cristiano Ronaldo.(BBC Sport)
Ibrahimovic:Mshambuliaji wa PSG Mswedeni Zlatan Ibrahimovic ameripotiwa kuwa anafikiria kitimkia katika ligi kuu ya England huku Arsenal ikitajwa kuwa ni chaguo lake la kwanza.(Sunday Mirror)
Florenzi:Arsenal imeripotiwa kujiandaa kumwaga pesa hapo mwezi januari kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa kulia wa AS Roma Alessandro Florenzi lakini itabidi ipambane kwani FC Barcelona nayo inamtaka mlinzi huyo ili kuwa mbadala wa muda mrefu wa mlinzi Dani Alves. (Metro)
Berahino:Manchester United imeripotiwa kuwa tayari kumsajili staa wa West Brom Saido Berahino ifikapo mwezi januari mwakani.Berahino,22 ameifungia West Brom magoli 32 katika michezo 88.(Sun on Sunday)
Aubameyang:Chelsea inaandaa kitita cha £20m ili kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang ili kuongeza makali katika kikosi chake.Msimu huu Aubameyang amefunga magoli 20 katika michezo 22.(The Sun)
0 comments:
Post a Comment