London,England.
Kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amekiri maji kumfika shingoni baada ya kiungo wake tegemeo wa ulinzi Mfaransa Francis Coquelin kuripotiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitatu baada ya kupata jeraha la goti katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa jumamosi iliyopita dhidi ya West Bromwich Albion.
Akiongea na shirika la habari la Uingereza la Reuters Wenger amekiri kwamba kuumia kwa Coquelin ni pigo kubwa hasa katika kipindi hiki ambacho Arsenal inakabiliwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha inashinda michezo yake dhidi ya Dynamo Zagreb na Olympiakos na kutinga hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Wenger amesema "Tuna wachezaji ambao wanaweza kucheza mahala pa Coquelin [Francis],Calum Chambers akiwa mmoja wao lakini tunapaswa kufanya usajili januari japo januari huwa siyo kipindi kizuri sana cha usajili.Tutafanya kila kinachowezekana kuongeza watu kikosini"
0 comments:
Post a Comment