728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, November 26, 2015

    PLUIJM AJA NA STAILI YA CHINJA CHINJA YANGA


    UNAIJUA ile staili ambayo Barcelona imeitumia kuichinja Real Madrid kwenye El Clasico kwa kuwapiga bao 4-0? Basi ndiyo hiyo imeanza kutumiwa na kocha wa Yanga, Mholanzi Hans van Pluijm.
    Staili (mfumo) hiyo ambayo inajulikana kwa jina la ‘tiki taka’ ikihusisha kucheza soka la kasi na pasi fupi fupi za haraka imekuwa ikitumiwa na Barcelona na kuipa mafanikio makubwa, ndiyo Pluijm aliitumia kwenye mazoezi ya jana ya Yanga katika Uwanja wa Boko Veterani.
    Pluijm na msaidizi wake, Juma Mwambusi, wameonekana kutotaka mchezo katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama kupisha michuano ya kimataifa kwa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na sasa Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes ambazo hivi sasa zipo nchini Ethiopia zikishiriki michuano ya Chalenji.
    Takribani wiki ya pili vijana hao wa Jangwani wapo kwenye mazoezi makali ya kujiandaa na michuano ya ligi ambapo kwenye mazoezi hayo wachezaji wa kimataifa; Thaban Kamusoko, Mbuyu Twite, Donald Ngoma na Vicent Bossou wameonekana kujituma vilivyo na kuwakosha mashabiki wachache wanaohudhuria kuangalia mazoezi hayo.
    Katika mazoezi yaliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Boko Veterani na Pluijm na wasaidizi wake Mwambusi na Juma Pondamali walianza programu yao ya siku na mazoezi mepesi kabla ya kuanza kuwapa mbinu za kiufundi wachezaji wao.
    Kwenye mazoezi hayo, Pluijm aligawa vikosi viwili vya ushindani na kuanza kucheza ambapo aliwataka wachezaji wake kucheza kwa kugusa mpira mara moja tu, huku wengine wakikaba muda wote bila kuchoka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PLUIJM AJA NA STAILI YA CHINJA CHINJA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top