Addis Ababa,Ethiopia.
Burundi na Rwanda zimeianza vyema Michuano ya Cecafa Chalenji Cup baada ya jana jumamosi kuibuka na ushindi dhidi ya Zanzibar na Ethiopia.
Katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa katika dimba la Addis Ababa Burundi imekaa kileleni mwa kundi B baada ya kuilaza Zanzibar kwa bao 1-0.Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji Didier Kavumbagu dakika ya 39 kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Zanzibar Mwadini Ali Mwadini na kutinga wavuni.
Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo Rwanda imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Ethiopia.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa na Jacques Tuyisenge na kuipeleka Rwanda kileleni mwa kundi A.
Michezo mingine ya michuano hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo ambapo kutoka kundi B,Kenya itavaana na Uganda kisha Kilimanjaro Stars itashuka dimbani kuvaana na Somalia.
0 comments:
Post a Comment