Addis Ababa,Ethiopia.
Kilimanjaro Stars imemaliza michezo ya hatua ya makundi ya Cecafa baada ya jioni ya leo kutoka sare ya goli 1-1 na wenyeji Ethiopia katika mchezo wa kundi A uliopigwa katika dimba la Awassa.
Kilimanjaro Stars ilipata goli dakika ya 58 kupitia kwa Simon Msuva kabla ya Ethiopia kusawazisha dakika ya 92 kwa goli la kujifunga la mlinzi Salim Mbonde.
Katika mchezo mwingine Uganda imefuzu boro fainali baada ya kuifunga Burundi kwa bao 1-0 lililofungwa na Frank Kalanda dakika ya 70.
Wakati huohuo ratiba ya michuano ya robo finali imetolewa jioni ya leo ambapo Kilimanjaro Stars itavaana tena na Ethiopia.Ratiba iko kama ifuatavyo....
Jumatatu
Uganda v Malawi
Tanzania v Ethiopia
Jumanne
South Sudan v Sudan
Rwanda v Kenya
0 comments:
Post a Comment