London,England.
Chama cha soka England kikishirikiana na Serikali ya nchi hiyo kimeimarisha ulinzi katika uwanja wa Wembley ambao leo jumanne utachezewa mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya England na Ufaransa.
FA imechukua tahadhari hiyo kufuatia jiji la Paris,Ufaransa siku tano zilizopita kushambuliwa na magaidi katika siku ambayo Ufaransa ilikuwa ikicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ujerumani na watu wapatao 129 kufariki dunia kutokana na mashambulizi hayo.
Hivi ndivyo uwanja wa Wembley unavyoonekana baada ya ulinzi kuanza kuimarishwa ambapo mashabiki zaidi ya 70,000 wanatarajiwa kushuhudia mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment