728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, November 21, 2015

    VAN GAAL ASEMA ALIMNUNUA MCHEZAJI HUYU KWA PESA TOKA MFUKONI MWAKE


    Manchester, England.

    Meneja wa Manchester United Mdachi Louis van Gaal amefichua kwamba alimsajili staa wa zamani wa Nigeria Finidi George kwa pesa toka mfukoni mwake wakati huo akiifundisha Ajax ya nyumbani kwao Uholanzi.

    Van Gaal, 64, aliyehudumu Amsterdam Arena (Ajax) kwa miaka sita na kufanikiwa kutwaa mataji mbalimbali 11 ikiwemo taji la Ulaya 1995 amesema hali ngumu ya kiuchumi katika klabu hiyo ilimlazimu afanye usajili kwa pesa yake mwenyewe ili kuweka mambo sawa.

    Akiongea na Daily Telegraph,Van Gaal amesema 

    “Hatukuwa na pesa yoyote wakati huo,tulikuwa tumefirisika kabisa.Hatukuwa na uwezo wa kununua mastaa,kimbilio lilikuwa ni kuwageukia vijana/makinda.

    "Tulimnunua Jari Litmanen kwa £10,000.Pia tukamnunua Finidi George mwaka 1993 kutoka Sharks ya Nigeria.Alikuwa anauzwa kwa £3,000 pesa ambayo niliitoa mfukoni mwangu kisha tukamnunua Marc Overmars"Alimaliza Van Gaal.

    Mwaka 1995 Ajax ilitwaa ubingwa wa Ulaya,Van Gaal akatimkia FC Barcelona mwaka 1997 huku Finidi George akijiunga na Real Betis mwaka 1996.


    Finidi George
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VAN GAAL ASEMA ALIMNUNUA MCHEZAJI HUYU KWA PESA TOKA MFUKONI MWAKE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top