728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, November 24, 2015

    SERGIO AGUERO AWEKA REKODI MPYA EPL

    Manchester, England.

    Mshambuliaji wa Manchester City Muargentina Sergio Aguero ameweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Amerika Kusini kufunga magoli mengi katika ligi kuu ya England baada ya kufikisha magoli 85 tangu kuasisiwa kwa ligi hiyo maarufu duniani.

    Aguero aliyejiunga na Manchester City mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid alifikisha idadi hiyo siku ya jumamosi baada ya kufunga goli moja katika mchezo ambao Manchester City ililala kwa magoli 4-0 toka kwa Liverpool.

    Goli hilo la dakika ya 44 limemfanya Aguero ampiku raia mwenzie wa Argentina Carlos Tevez mwenye magoli 84 huku Louis Suarez akifuatia baada ya kufunga magoli 69.

    Orodha kamili iko kama ifuatavyo......

    1. Aguero - 85 
    2. Tevez - 84 
    3. Suarez - 69 
    4. Poyet - 54 
    5. Solano - 49 
    6. Angel - 44 
    7. Ricard - 31 
    8. Juninho - 29 
    9. Rodallega - 29 
    10. Cort - 28 



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SERGIO AGUERO AWEKA REKODI MPYA EPL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top