728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, November 28, 2015

    LA LIGA:BARCELONA YAINYONGA REAL SOCIEDAD NNE MTUNGI

    Barcelona,Hispania.

    Barcelona imeendelea kutoa vipigo kwa wapinzani wake baada ya jioni ya leo kuitandika Real Sociedad kwa mabao 4-0 katika mchezo wa ligi ya La Liga uliopigwa katika dimba la Camp Nou.

    Barcelona imejipatia magoli yake dakika za 22 na 53 kupitia kwa Neymar Jr kisha dakika ya 41 kupitia kwa Louis Suarez na Lionel Messi dakika ya 91.

    Baada ya ushindi huo Barcelona imeendelea kujikita kileleni mwa ligi ya La Liga baada ya kujikusanyia pointi 33 katika michezo 13.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LA LIGA:BARCELONA YAINYONGA REAL SOCIEDAD NNE MTUNGI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top