Paris,Ufaransa.
Shirikisho la vyama vya soka barani Ulaya (UEFA) limetoa orodha ya wachezaji 40 watakaowania kuingia katika kikosi chake cha wachezaji nyota 11 bora wa mwaka.
Katika orodha hiyo iliyotolewa jana jumanne FC Barcelona imeongoza kwa kutoa nyota wengi zaidi,imetoa nyota wanane ikifuatia na Bayern Munich iliyotoa nyota watano,ligi kuu ya Uingereza kwa ujumla wake ikitoa nyota watano tu huku Gareth Bale na Joe Hart wakiwa ni wachezaji pekee raia wa Uingereza waliofanikiwa kuingia katika kinyang'anyiro hicho.
Orodha hiyo iliyojumuisha magolikipa wanne,walinzi 12,viungo 12 na washambuliaji 12 imetolewa kwa kuzingatia viwango vilivyoonyeshwa na wachezaji husika kwa mwaka mzima wa 2015 na maamuzi ya wachezaji gani wanastahili kuwemo katika kikosi cha mwaka hufanywa na mashabiki ambao hupiga kura kupitia mtandao wa shirikisho hilo wa Uefa.com.Kikosi hicho cha wachezaji bora 11 kitatangazwa januari 5 mwakani.
Orodha kamili iko kama ifuatavyo......
Magolikipa:Joe Hart (Manchester City),Gianluigi Buffon (Juventus), Manuel Neuer (Bayern Munich), Denys Boyko (Dnipro).
Walinzi:Leonardo Bonucci (Juventus),David Alaba (Bayern Munich), Giorgio
Chiellini (Juventus), David Luiz (Paris Saint-Germain), Dani Alves (Barcelona),
Thiago Silva (Paris Saint-Germain), Jérôme Boateng (Bayern Munich), Ricardo Rodríguez (Wolfsburg), Javier Mascherano (Barcelona), Diego Godin (Atlético Madrid),
Gerard Piqué (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid).
Viungo:Grzegorz Krychowiak
(Sevilla), Kevin De Bruyne (Manchester City), Ivan Rakitic (Barcelona), Arturo
Vidal (Bayern Munich), Eden Hazard (Chelsea), Claudio Marchisio (Juventus),
Marco Verratti (Paris Saint-Germain),Yevhen Konoplyanka (Sevilla), Andrés
Iniesta (Barcelona), James Rodríguez (Real Madrid), Paul Pogba (Juventus), Hakan
Calhanoglu (Bayer Leverkusen).
Washambuliaji:Gareth Bale (Real Madrid),Thomas Müller (Bayern Munich), Lionel
Messi (Barcelona), Zlatan Ibrahimovic (Paris Saint-Germain), Robert Lewandowski (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Antoine Griezmann (Atlético
Madrid), Álvaro Morata (Juventus), Sergio Agüero (Manchester City), Luis Suárez (Barcelona), Alexis Sánchez (Arsenal),Cristiano Ronaldo (Real Madrid).
0 comments:
Post a Comment