Paul Manjale.
Rodgers:Kocha wa zamani wa Liverpool Brendan Rodgers yuko nchini Qatar kwa mazungumzo ya awali kabla ya kusaini mkataba wenye thamani ya £3.5m wa kuinoa Al Sadd. (The Sun)
Seedorf:Newcastle imefanya mazungumzo na kocha wa zamani wa AC Milan Clarence Seedorf kuhusu uwezekano wa kuinoa klabu hiyo inayojipanga kumtupia virago kocha wake Steve McClaren kufuatia mwenendo mbaya kwenye ligi.(Calciomercato)
Calleri:Chelsea imewekwa mkao wa kula na Boca Juniors baada ya miamba hiyo ya Argentina kusema iko tayari kumuuza straika wake hatari Jonathan Calleri aliyefunga magoli 21 msimu uliopita na kuiwezesha kutwaa ubingwa.(AS)
Koziello:Arsenal imeipiku Chelsea katika mbio za kuisaka saini ya kiungo kinda wa Nice Vincent Koziello,20 baada ya kuripotiwa kuanza mazungumzo ya kumsajili kiungo huyo Mfaransa ili kuja kuziba nafasi ya Francis Coquelin aliyeumia.(Canal +)
Kane:Tottenham inajipanga kutumia kitita cha £25m ili kuwashawishi nyota wake wawili Harry Kane na Dele Alli waendelee kukipiga White Hart Lane kwa kuwaboreshea mishahara yao na marupurupu mengine.Kane atapandishiwa mshahara kutoka £45,000 mpaka £70,000 kwa wiki huku Alli akipandishiwa kutoka 12,500 mpaka £25,000 kwa wiki.(Sun)
Dembele:Manchester United imetajwa kuwa ni moja kati ya vilabu vinavyomuwania mshambuliaji kinda wa Fulham Moussa Dembele mwenye miaka 19.(Daily Mirror)
Boufal:Liverpool na Tottenham wanakabiliwa na upinzani mkali toka kwa Paris Saint-Germain katika mbio za kumsajili winga wa Lille Sofiane Boufal hapo mwezi januari.(Daily Express)
Perotti:Arsenal imeongeza mbio za kumsaka winga mwenye kasi wa Genoa Muargentina Diego Perotti,27 ili kuongeza makali katika safu yake ya ushambuliaji inayokabiliwa na wimbi la majeruhi.Arsenal iko tayari kutoa £9.8m ili kumnasa nyota huyo wa zamani wa Sevilla.(Metro)
0 comments:
Post a Comment