Stockholm, Sweden.
Timu ya taifa ya Sweden imeanza vyema kuisaka tiketi ya kufuzu michuano ijayo ya Ulaya (Euro 2016) baada ya kuilaza Denmark kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano uliopigwa katika dimba la Friends Arena,Stockholm (Sweden).
Sweden ilipata mabao yake kupitia Emil Forsberg aliyefunga bao la kuongoza dakika ya 45 kisha nahodha Zlatan Ibrahimovic kuongeza la pili dakika ya 50 kwa mkwaju wa penati.
Penati hiyo ilitolewa baada ya Thomas Kahlenberg wa Dermark kumfanyia madhambi katika eneo la hatari Emil Forsberg na Ibrahimovic kufunga kumfunga kirahisi Kasper Schemeikel.
Denmark ikionekana kama itaondoka Friends Arena ikiwa nyuma kwa bao 2-0 iliamka dakika ya 80 na kujipatia bao la kufutia machozi kupitia kwa Nicolai
Jorgensen.
Miamba hiyo ya Scandinavia ililazimika kucheza hatua hiyo ya mtoano baada ya kushindwa kufuzu moja kwa moja katika hatua za makundi baada ya kushika nafasi za tatu katika makundi yao.
Sweden na Denmark zitavaana tena Novemba 17 jijini Copenhagen ili kuipata timu moja itayofuzu Euro 2016 huko Ufaransa.
VIKOSI
Sweden: 1-Isaksson (GK) 2 Lustig 3-Antonsson 4 Granqvist 5-M Olsson 6 Forsberg 8-Lewicki 9 Källström 21-Durmaz 10-Ibrahimović (C) 19-Berg.
Denmark: 1-Schmeichel (GK) 3-Kjær 4-Agger (C),5-Durmisi 6-Jacobsen 7-Kvist,10-Eriksen 15-Kahlenberg,8 Braithwaite,11-Bendtner 21-Fischer.
0 comments:
Post a Comment