728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, November 20, 2015

    MSHINDWE WENYEWE:CHELSEA YAAMBIWA ITOE £30M TU IPEWE STRAIKA ANAYEONGOZA KWA MAGOLI ULAYA,COUTOIS AANZA MAZOEZI


    Donestik,Ukraine.

    CHELSEA imeambiwa inaweza kuinasa saini ya straika wa Shakhtar Donetsk Mbrazil Alex Teixeira ikiwa itakuwa tayari kutoa kitita cha £30m kinachotakiwa na klabu hiyo ya Ukraine.

    Siku za hivi karibuni Chelsea imekuwa ikimfuatilia kwa karibu Texeira,25 ili kuongeza makali katika safu yake ya ushambuliaji ambayo kwa msimu huu imekuwa butu kiasi cha kukatisha tamaa.

    Texeira aliyejiunga na Shaktar Donestik mwaka 2010 akitokea Vasco Da Gama ya nyumbani kwao Brazil ndiye mfungaji kinara kwasasa Ulaya baada ya kufunga magoli 21 katika michezo 22.

    Wakati huohuo Chelsea imepata afueni baada ya mlinda mlango wake namba moja Thibaut Courtois kurejea mazoezini jana alhamis.

    Courtois,23 aliyekuwa nje ya dimba tangu Agosti kufuatiwa kufanyiwa upasuaji katika goti lake amefanikiwa kumaliza vizuri siku ya kwanza mazoezini na huenda akarejea langoni mwezi Disemba.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MSHINDWE WENYEWE:CHELSEA YAAMBIWA ITOE £30M TU IPEWE STRAIKA ANAYEONGOZA KWA MAGOLI ULAYA,COUTOIS AANZA MAZOEZI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top