London,England.
ARSENAL imelazimishwa sare ya goli 1-1 na Norwich City katika mchezo wa ligi kuu nchini England uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Carrow Road huko Norwich.
Mesut Ozil alianza kuifungia Arsenal goli la kuongoza dakika ya 30 akiiwahi pasi ya Alexis Sanchez na kumfunga kwa urahisi mlingo wa Norwich City John Ruddy.
Norwich City ilifanikiwa kusawazisha goli hilo kupitia kwa Lewis Grabban dakika ya 43 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Arsenal na kumchambua mlinda mlango Peter Cech.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo uliopigwa huko Anfield goli la mkwaju wa penati ya kiungo James Milner limeipa Liverpool ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Swansea City.
Goli hilo lilipatikana baada ya mlinzi wa Swansea City Ryan Taylor kuunawa ndani ya eneo la mpira uliopigwa Jordan Ibe na mwamuzi kuamuru ipigwe penati iliyofunga na Milner kwa shuti kali la juu.
0 comments:
Post a Comment