Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Stand United na kinara wa mabao katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Elius Maguli ameitaka Simba kumpa dau la Sh50 milioni ili kumwaga wino wa kuichezea klabu hiyo.
Maguli alikuwa akisugua benchi ndani ya klabu hiyo ya Msimbazi, huku akiaminika amekwisha na wekundu hao kumsajili Musa Hassan ‘Mgosi’ na Pape N’daw, ambao hadi ligi inasimama hawana bao hata moja.
Maguli, ambaye aliachwa Simba licha ya kufunga mabao manne katika mechi za kirafiki, alikaririwa akisema kuwa yupo tayari kumwaga wino ndani ya wekundu hao wa Msimbazi iwapo watampa kiasi hicho cha fedha na kwamba kama fedha hizo hazipo wasahau yeye kurudi tena Msimbazi.
0 comments:
Post a Comment