London,England.
Arsenal imeshinda vita ya kuituliza akili ya nyota wake Mchile Alexis Sanchez baada ya kufanikiwa kumshawishi kusaini mkataba mpya wa miaka mitano.
Mkataba huo wenye thamani ya £40m utamuwezesha Sanchez,26 kuvuna mshahara wa £150,000 kwa wiki toka ule wa £130,000 anaouvuna sasa.
Arsenal imeamua kumpa Sanchez mkataba mpya na wenye maslahi mazuri ili kuzima ndoto za vilabu vya Real Madrid na Manchester United ambavyo siku za hivi karibuni viliripotiwa kuanza kummezea mate nyota huyo wa zamani wa FC Barcelona na Udinese ya Italia.
Wakati huohuo Arsenal pia imeripotiwa kuwa katika mazungumzo na kiungo wake Mesut Ozil kwa ajili ya kurefusha mkataba wake
0 comments:
Post a Comment