728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, November 14, 2015

    KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018:STARS YABANWA NA ALGERIA,YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 U/TAIFA,WALINZI WABOA

    Dar es salaam,Tanzania.

    Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya bao 2-2 na timu ya taifa ya Algeria katika mchezo mkali wa kuwania tiketi ya kuingia hatua ya makundi ya kuwania nafasi ya kucheza michuano ya kombe la dunia huko Urusi mwaka 2018.

    Stars ambayo ilikuwa imeweka kambi yake Afrika Kusini kwa karibia majuma mawili ilionyesha kuimudu kwa kiasi kikubwa Algeria na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 43 kupitia kwa mshambuliaji Elias Maguli aliyefunga kwa kichwa safi akiunganisha krosi ya mlinzi Hadji Mwinyi Mngwali.

    Kuingia kwa bao kuliipa nguvu Stars kwani dakika ya 54 mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta alifunga goli la pili baada ya kuwachambua walinzi wa Algeria na kumfunga kirahisi mlinda mlango Rais Mbohli.

    Kuingia kwa bao hilo la pili kuliiamsha Algeria ambayo ilifanikiwa kusawazisha mabao hayo kupitia kwa mshambuliaji Sliman Islam dakika za 71 na 75.

    Islam alifunga mabao hayo kufuatia walinzi wa Stars kujichanganya na kupoteza umakini kadri muda ulivyokuwa unakwenda na kuufanya mchezo huo umalizike kwa sare ya mabao 2-2.

    Kufuatia matokeo hayo Stars inakabiriwa na kazi ngumu katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Novemba 17 huko Algers,Algeria. 



     

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018:STARS YABANWA NA ALGERIA,YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 U/TAIFA,WALINZI WABOA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top