Dar es salaam,Tanzania.
Beki wa pembeni wa Simba, Hassani Kessy, amefunguka na kutaja sababu inayomzuia asiongeze mkataba ni timu
hiyo kutoshiriki michuano ya kimataifa Afrika.
Kufikia mwezi ujao, Kessy atakuwa amebakiza miezi sita katika mkataba wake na kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa),anaruhusiwa kufanya mazungumzo na
klabu nyingine inayomhitaji ikiwemo Yanga ambayo inatajwa kumuwania kwa
ukaribu.
Yanga itashiriki katika Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.
Kessy amesema mipango aliyojiwekea ni kucheza soka la kimataifa nje ya Tanzania na ndiyo maana amekuwa
akisita kusaini mkataba mpya Simba.
“Sifikirii kuongeza mkataba wa kubaki kuendelea kuichezea Simba katika kipindi kingine, licha ya viongozi kuhitaji huduma yangu.
“Ninaamini kama nikipata timu inayoshiriki michuano ya kimataifa, basi bila kuchelewa nitasaini mkataba ili iwe
rahisi kwaku kutimiza ndoto zangu kwa kuwa nitaonekana kimataifa,” alisema Kessy.
0 comments:
Post a Comment