728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, November 27, 2015

    ZANZIBAR HEROES YAAGA CHALENJI KWA KUISHUSHIA KIPIGO KIKALI KENYA

    Addis Ababa,Ethiopia.

    Zanzibar heroes imeyaanga mashindano ya Cecafa yanayoendelea huko Ethiopia kwa kuishushia Kenya kipigo cha magoli 3-1 katika mchezo mkali wa kundi B uliopigwa jioni ya leo huko Awassa,Ethiopia.

    Zanzibar heroes ambayo iliianza michuano ya mwaka huu kwa kupokea vichapo toka kwa Burundi kisha Uganda leo ilionekana kuamka na kuizidi ujanja Kenya karibu kila idara.

    Magoli ya Zanzibar Heroes yamepachikwa kimiani na Suleimani kisha Hamis Mcha kuongeza mengine mawili huku Kenya ikipata goli lake kupitia kwa Jacob Keli.

    Kufuatia ushindi huo Zanzibar heroes imefanikiwa kulifuta gundu la kutoifunga Kenya kwa miaka 35.Mara ya mwisho Zanzibar Heroes Kuifunga Kenya ilikuwa ni Novemba 11 mwaka 1980.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ZANZIBAR HEROES YAAGA CHALENJI KWA KUISHUSHIA KIPIGO KIKALI KENYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top