Kampala,Uganda.
Timu ya taifa ya Uganda (Cranes) leo imekata tiketi ya kuingia hatua ya makundi ya kusaka nafasi ya kushiriki kombe la dunia mwaka 2018 baada ya kuilaza Togo kwa mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa katika dimba la Nelson Mandela jijini Kampala.
Uganda ambayo katika mchezo wa kwanza iliilaza Togo kwa bao 1-0 ugenini jijini Rome leo ilikuwa na kazi rahisi ya kujihakikishia ushindi kwani ilitumia dakika 5 tu kupata bao la kuongoza baada ya shuti kali la mita 20 la nahodha Geoffrey Massa kumshinda mlinda mlango wa Togo Djehani Gussad na kujaa wavuni.
Baada ya kuingia kwa bao hilo hilo Uganda haikuonyesha kuridhika kwani iliendelea kuichachafya Togo na kujipatia mabao mengine mawili kupitia kwa Farouk Miya aliyefunga dakika za 41 na 45 na kuihakikishia Uganda ushindi wa jumla wa mabao 4-0 na kutinga hatua ya makundi.
VIKOSI
Uganda XI: Onyango, Jjuuko, Isinde, Mawejje,Ochaya, Khalid (Kizito 27'), Kizito (Umony 74'), Miya, Iguma, Walusimbi (Oloya 63'),Massa.
Togo XI: Djehani, Akakpo (Fessou 25'),Mamah, Ouro-Akoriko, Djene, Dossevi (Mawuena 69'), Nouwoklo, Gakpe, Eninful,Wome,Amevor.
Katika mchezo mwingine Zambia nayo imefuzu baada ya kuitungia Sudan kwa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa katika dimba la Levy Mwanawasa,Ndola.
Magoli ya wenyeji Zambia yamefungwa na Lubambo Musonda na Winston Kalengo na kufuzu kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya mchezo wa kwanza kuibuka kidedea kwa bao 1-0 huko Sudan.
Huko Gabon,timu ya taifa hilo nayo imefuzu baada ya kuibajua Msumbiji kwa mikwaju ya penati.
Stars itarudiana na Algeria jumanne hii huko Algers,Algeria baada ya kutoka sare ya 2-2 Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment