Johannesburg, Afrika Kusini.
Shirika la habari la Uingereza (BBC) leo jumamosi limetoa orodha ya wachezaji watano watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa mwaka 2015.
Tuzo hiyo inayoshikiliwa na nyota wa Algeria Yacine Brahimi itatolewa Desemba 11 huko Johanneaburg,Afrika Kusini ambapo mshindi atatokana na kura zitakazopigwa na mashabiki kupitia ujumbe mfupi wa simu za mikononi na internet.Mwisho wa kupiga kura ni Novemba 30.
Orodha kamili ya nyota wanawania tuzo hiyo ni Andre Ayew (Ghana),Yacine Brahimi (Algeria), Yaya Toure (Ivory Coast), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon) na Sadio Mane (Senegal).
Nyota waliowahi kuitwaa tuzo hiyo ni Austin Okocha, Yaya
Toure, Abedi Pele, George Weah,Kalusha Bwalya,Emmanuel Amuneke,Nwankwo Kanu, Patrick Mboma, Michael Essien na Emmanuel Adebayor na Yacine Brahimi.
0 comments:
Post a Comment