728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, November 18, 2015

    MAGULI RASMI YANGA


    KAMA ulikuwa hufahamu, basi fowadi ya timu ya Yanga sasa itakuwa noma. Hii ni baada ya kudhihirika kwamba straika wa Stand United, Elias Maguli, atasaini rasmi kukipiga katika kikosi cha timu hiyo ya Jangwani baada ya kuonyesha uwezo mkubwa katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na timu ya Taifa 'Taifa Stars.'

    Hata hivyo, mashabiki wa Yanga itabidi wavute subira kidogo kwani mchezaji huyo atatua Jangwani mara baada ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

    Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinadai kuwa straika huyo ametengewa dau la shilingi milioni 40 aliloliomba na kinachosubiriwa ni kumalizika kwa ligi ili Wanajangwani hao wapate wasaa mzuri wa kukaa meza moja na viongozi wa Stand United.

    "Hakuna shaka kwamba, Maguli ataichezea Yanga ila mipango ni msimu ujao na tayari ameshatengewa dau na hata yeye mwenyewe anapenda kuchezea klabu kubwa kama hii," kilisema chanzo cha habari hizi.

    Japo baadhi ya viongozi wa Yanga wameshindwa kusema moja kwa moja juu ya suala hilo, lakini DIMBA linafahamu kuwa mipango ipo na inaweza kutekelezwa kwani Wanajangwani hao wanapoamua jambo, hakuna wa kuwazuia.


    (CHANZO:BINGWA)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAGULI RASMI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top