728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, November 19, 2015

    MPAKA KIELEWEKE:MASHABIKI ARSENAL WAJIPANGA KULIPA MSHAHARA WA MESSI ILI ATUE EMIRATES


    London,England.

    Unaikumbuka ile habari ya Lionel Messi kuwa tayari kujiunga na Arsenal ikiwa ataamua kuachana na FC Barcelona.Unaukumbuka pia ule mshahara wa £600,000 atakaotaka kulipwa kila wiki???

    Sasa mashabiki wa Arsenal wameamua kulivalia njuga suala hilo ili kuhakikisha kuwa klabu yao haimkosi kwa mara nyingine mshindi huyo wa tuzo nne za mchezaji bora wa dunia (Ballon d'Or) baada ya kuonyesha dalili za kutaka kuisaidia kulipa mshahara wa nyota huyo toka Argentina.

    Shabiki mmoja wa kutupwa wa Arsenal aitwaye Matt Clark kupitia ukurasa wake wa twitter amekuja na wazo la kutaka mashabiki wapatao 599,999 wa klabu hiyo kila mmoja kuchangia £1 kila wiki kwa ajili ya kulipa mshahara wa Lionel Messi huku Arsenal ikiachiwa kushughulikia dau la uhamisho peke yake.

    Mapema wiki iliyopita magazeti mbalimbali ya michezo ya England na Hispania yaliripoti kuwa Lionel Messi atapendelea kucheza Arsenal ikiwa ataamua kuachana na FC Barcelona.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MPAKA KIELEWEKE:MASHABIKI ARSENAL WAJIPANGA KULIPA MSHAHARA WA MESSI ILI ATUE EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top