728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, November 23, 2015

    BAADA YA KICHAPO CHA GOLI NNE,RIVALDO AIPA UJANJA REAL MADRID

    Sao Paulo,Brazil.


    Nyota wa zamani wa FC Barcelona Mbrazil Rivaldo Vitor Borba Ferreira ameipa ujanja Real Madrid ambao utaisaidia kujiepusha na tabia ya kutimua na kuajiri makocha kila kukicha.

    Rivaldo ambaye jumamosi alikuwa nyumbani kwao Brazil akiufuatilia mchezo wa  "El Classico"  kupitia luninga ameitaka Real Madrid kutoenda mbali kumtafuta mrithi wa Rafael Benitez ikiwa itaamua kumfukuza kwani tayari wanaye Zinedine Zidane ambaye tayari amewiva na anaweza kuiletea mafanikio klabu hiyo ikiwa atamuamini.
     

    Rivaldo ameitaka Real Madrid kurudi nyuma na kujifunza toka kwa FC Barcelona ambayo imekuwa na kawaida ya kuwapa nafasi ya ukocha nyota wake wa zamani.

    Amesema "Real Madrid wanapaswa kumuamini Zidane na kumpa jukumu la ukocha mkuu.Alikuwa msaidizi wa Carlo Ancelotti  msimu uliopita,naamini amejifunza mengi.Muda wa kumpa nafasi ndiyo huu.Nadhani huu ni wakati wa kumuamini,kama ambayo Barca imefanya kwa Pep Guardiola na Luis Henrique"Alimaliza Rivaldo.
     



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAADA YA KICHAPO CHA GOLI NNE,RIVALDO AIPA UJANJA REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top