London,England.
Arsenal imefufua matumaini ya kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya vilabu bingwa barani Ulaya baada ya usiku wa leo kuilaza Dynamo Zagreb kwa jumla ya mabao 3-0.
Arsenal ikiwa katika dimba lake la nyumbani la Emirates imepata magoli yake kupitia kwa Mesut Ozil na Alexis Sanchez aliyefunga mara mbili.
Kufuatia ushindi huo Arsenal inakuwa imefikisha pointi sita ikihitaji kuifunga Olympiacos ambayo leo imekutana na kichapo cha mbwa mwizi baada ya kubamizwa magoli 4-0 na Bayern Munich katika mchezo uliopigwa katika dimba la Allianz Arena.
Magoli ya Bayern Munich yamefungwa na Douglas Costa,Robert Lewandowski,Thomas Muller na Kingsley Coman huku mlinzi Holger BudStuber akilimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
Katika mchezo mwingine Chelsea imeifunga Maccabi Tel Aviv kwa jumla ya magoli 4-0 wafungaji wakiwa ni Garry Cahill,Willian,Oscar na Kurt Zouma.
Kwingineko Barcelona imeinyuka AS Roma kwa jumla ya magoli 6-1.Magoli ya Barcelona yamefungwa na Louis Suarez aliyefunga mawili,Lionel Messi,Adriano Correa na Gerrard Pique huku Edin Dzeko akiifungia AS Roma goli la kufutia machozi.
Matokeo mengine
Zenit St 2-0 Valencia
BATE 1-1 Bayer Leverkusen
Porto 0-2 Dynamo Kiev
Lyon 1-2 Genk
0 comments:
Post a Comment