Awassa City, Ethiopia.
Timu za soka za Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes leo zitakuwa na vibarua vigumu pale zitakaposhuka dimbani kuvaana na Rwanda na Uganda katika michuano inayiendelea ya Cecafa Chalenji Cup.
Katika mchezo wa kwanza utakaopigwa saa 8:00 mchana Zanzibar Heroes itashuka dimbani kuvaana na Uganda Cranes.Timu zote zinaingia katika mchezo wa leo zikiwa na kumbukumbu ya kupoteza katika mechi za ufunguzi.
Zanzibar Heroes ilifungwa 1-0 na Burundi wakati Uganda iliambulia kichapo cha magoli 2-0 toka kwa wapinzani wao wa jadi Kenya.
Katika mchezo wa pili utakaopigwa saa 12:00 jioni Kilimanjaro Stars ambayo katika mchezo wake wa kwanza iliibanjua Ethiopia kwa magoli 4-0 itapimana ubavu na timu ngumu ya Rwanda.
0 comments:
Post a Comment