728x90 AdSpace

Thursday, November 26, 2015

MOURINHO AELEZA KWANINI ANATAKA ARSENAL ITUPWE NJE YA MICHUANO YA LIGI YA MABINGWA ULAYA

London,England.


Watoke tu!!Hii ni kauli ya kocha Jose Mourinho baada ya kudai kuwa anatamani kuiona Arsenal ikitupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa pindi itakapovaana na Olympiacos katika mchezo wa mwisho wa kundi F hapo mwezi wa Disemba.

Mourinho ambaye siku ya jumanne aliiongoza klabu yake ya Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv ya Israel amesema ipo sababu kubwa inayofanya aiombee mabaya Arsenal.

Sababu hiyo ni kuwa kocha wa Olympiacos Marco Silva ni rafiki yake mkubwa hivyo yuko nyuma yake kuhakikisha anafanikiwa kuitoa Arsenal na kuisukumia katika michuano ya Europa Ligi.

Kwa kipindi kirefu sasa Mourinho amekuwa hana mahusiano mazuri na Arsenal hasa kocha wake mkuu Arsene Wenger hali ambayo imewalazimu kuingia katika ugomvi wa mara kwa mara.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MOURINHO AELEZA KWANINI ANATAKA ARSENAL ITUPWE NJE YA MICHUANO YA LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown