728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, November 27, 2015

    FABREGAS:KIKWAZO MESSI

    London,England.

    Kiungo wa Chelsea Muhispania Cesc Fabregas ametazama jinsi Neymar Jr alivyoibeba Barcelona wakati Messi anaumwa na kukiri kuwa nyota huyo ni moto lakini akasisitiza ufalme wake utaanza rasmi siku Messi atakapokuwa amestaafu.

    Akiongea na mtandano wa Goal.Com Fabregas ambaye alicheza na Neymar Jr kwa msimu mmoja FC Barcelona klabu ya kutua Chelsea amesema Neymar Jr ni mfalme ajaye baada ya Messi kusema imetosha.

    "Neymar Jr ni moto,ana kipaji cha asili.Ana vitu vingi ambavyo wengine hawana.Ameonyesha hilo wakati Messi yuko nje"

    Akiulizwa kama anadhani Neymar Jr atakuja kufikia kiwango cha Messi amejibu "Nafikiri itakuwa ngumu kufika alipofika Messi lakini nadhani ufalme wake utaanza siku Messi atakapokuwa amestaafu.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: FABREGAS:KIKWAZO MESSI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top