Bilda,Algeria.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager,leo jumanne kitashuka katika dimba la Stade Mustapha Tchaker El Bouleïda,Bilda kuwavaa Algeria katika mchezo wa mkondo wa pili wa kuwania tiketi ya kuingia katika hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 huko Urusi.
Mchezo huo unaotarajiwa kuwa wa vuta nikute utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Mali na utaanza saa 1:15 usiku (Algeria) sawa na saa 3:15 usiku kwa saa nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki.
Wakati huo huo nyota wa Algeria Yacine Brahimi amerejea kikosini baada ya kukosekana katika mchezo wa kwanza kufuatia kusumbuliwa na majeraha ya misuli.
0 comments:
Post a Comment