Habari na Paul Manjale
Bellerin:Mlinzi wa kulia wa Arsenal Hector Bellerin,20 amesema klabu hiyo haina sababu ya kufanya usajili mwezi januari kwani kikosi kilichopo ni kizuri na kina uwezo wa kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.(Maily on Sunday)
Butland:Liverpool inaanda kitita cha £20 kwa ajili ya kumsajili kipa wa Stoke City Muingereza Jack Butland,22 baada ya kutoridhishwa na kiwango cha kipa wake namba moja Simon Mignolet.(Sun)
Mourinho:Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ana siku 14 tu za kuamua amsajili mshambuliaji yupi katika Jamie Vardy wa Leiceister City ama Saido Berahino wa West Bromwich ili kuongeza makali katika klabu yake ambayo msimu huu imeshindwa kufurukuta.
Vanja:Mlinda mlango kinda Mserbia Vanja Milinkovic-Savic,18 amevunja mkataba wake katika klabu ya Manchester United ikiwa ni miezi 18 tu tangu ajiunge nayo baada ya kushindwa kupata kibari cha kufanyia kazi nchini England.(Metro)
Stones:Arsenal imeripotiwa kuungana na Chelsea katika mbio za kuitaka saini ya mlinzi wa Everton John Stones,21 ambaye thamani yake ni zaidi ya £30m.(Metro)
Texeira:Mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk Mbrazil Alex Teixeira amesema Chelsea imeanza mazungumzo ya kutaka kumsajili hapo mwezi januari.Texeira,25 amefunga magoli 23 katika michezo 23.(Daily Mirror)
Townsend:Spurs iko tayari kumtoa winga wake Andros Townsend,24 pamoja na £25m ili kuinasa saini ya mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino,22.
Klopp:Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema yuko huru kusajili mchezaji yoyote yule toka klabu yake ya zamani Borussia Dortmund na hakuna makubaliano yoyote yanayoweza kukwamisha mpango huo.(Build)
Embolo:Vilabu vya Arsenal na Spurs vimeingia vitani vikisaka kuinasa saini ya mshambuliaji kinda wa FC Basle Breel Embolo mwenye asili ya Cameroon.Embolo,18 ameifungia Basle magoli 24 katika michezo 67 na thamani yake ni £21m.
0 comments:
Post a Comment