Munich,Ujerumani.
Nyota wa Bayern Munich Thomas Müller ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza mdogo zaidi kuwahi kushinda michezo 50 ya ligi ya mabingwa wa Ulaya tangu kuasisiwa kwake miaka mingi iliyopita.
Muller ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Bayern Munich kilichoibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Olympiacos jana jumanne ameweka rekodi hiyo akiwa na umri wa miaka 26,miezi miwili na siku 11 na kumpiku nyota wa zamani wa Real Madrid Muhispania Raul Gonzalez ambaye alifikisha idadi kama hiyo akiwa na umri wa miaka 26 na siku 257.
Nyota wengine waliowahi kushinda michezo 50 ya ligi ya mabingwa wakiwa na umri mdogo zaidi ni Lionel Messi (miaka 27,miezi minne na siku 12) pamoja na Cristiano Ronaldo (miaka 28 na mwezi mmoja)
0 comments:
Post a Comment