728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, November 16, 2015

    CECH ACHOKA KUCHEZA AKIWA AMEVAA HELMET,MADAKTARI WAMUONYA

    London,England.

    Petr Cech amefichua kwamba anataka kuanza kucheza bila ya kuvaa helmet kichwani mwake lakini amekutana na upinzani mkali toka kwa madaktari wake. 

    Mlinda mlango huyo wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa anakipiga na Arsenal amekuwa akivaa helmet tangu mwaka 2006 baada ya kupata mpasuko katika fuvu la kichwa chake kufuatia kugongana na kiungo wa Reading Nicky Hunt tukio lililofanya awe nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.

    Cech , 33,amesema kuwa amechoka kuvaa helmet akidai kuwa inampunguzia kujiamini na hata kufanya mawasiliano kati yake na wachezaji wenzake uwanjani kuwa magumu kutokana na masikio yake kuwa yamezibwa.

    Amesema "Ningekuwa najiamini sana kama nisingekuwa navaa helmet.Kama unapenda ama hupendi,helmet inaathiri sana mazingira yangu.Madaktari wameniambia niendelee kuvaa ili niendelee kuwa salama.

    Wakati huo huo Cech amekiri kuwa uvaaji wa helmet umemsaidia kwani ameshakutana na matukio mengine mawili ya kugongwa kichwani lakini akabaki salama. 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CECH ACHOKA KUCHEZA AKIWA AMEVAA HELMET,MADAKTARI WAMUONYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top