Mbali ya mshambuliaji Mbrazil Geilson Santos ” Jaja”kutawala
midomoni mwa mashabiki wa soka nchini baada ya kufunga goli mbili na kuiwezesha
klabu yake ya Yanga kutwaa Ngao ya Jamii kwa jumla ya goli 3-0 dhidi ya klabu
ya Azam katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa taifa jumapili iliyopita jina
jingine ambalo liingia kwa kasi midomoni mwa wapenda soka lilikuwa ni jina la
shabiki maarufu Steven Charles maarufu kama Steve Yanga baada ya kutinga
uwanjani hapo akiwa amevalia jezi ya Azam na kukaa mbali kabisa na jukwaa la
klabu ya Yanga.
Picha ya Steven iliyotibua hali ya hewa |
Mengi yameongelewa sana kuhusu kitendo cha shabiki huyo
ambaye huenda ndiye shabiki maarufu zaidi wa mpira kuliko wote nchini Tanzania
kwa miaka hii ya karibuni.Habari hizo ziliifikia timu makini ya MchakaMchaka
Viwanjani na hatimaye ikaanza kufanya mawindo ya chini kwa chini kumsaka na
kumtia mkononi shabiki huyo ili atueleze imekuwaje,Je ni mbwembwe tu kile
tunachokisikia ama ndiyo hali ilivyo?
Jumatatu asubuhi mwandishi wa habari hii alinyanyua simu na
kumtafuta Steve na maongezi yalikuwa hivi..
Steve akionyesha jeuri ya pesa |
Manjale:Mambo vipi Steve?
Steve:Manjale najua unachotaka kuongea
Manjale:Steve nasikia umeikimbia Yanga kaka imekuwaje?
Steve akiongoza kikundi mjengoni kwetu house kucheza mziki |
Steve:Mwanjala (hapa akachapia jina langu) ni maisha tu kaka.
Manjale:Steve naomba dakika chache tu unijibu maswali mawili
matatu niliyonayo hapa.
Steve:Kaka nina haraka kuna sehemu nawahi.(Simu ikakatwaa)
Mwandishi hakukata tamaa Jumanne mchana akampigia tena simu
lengo likiwa ni lile lile kuujua undani wa kile kinachoongeleka juu yake lakini
simu iliishia kukatwa na kuingia ujumbe mfupi usemao “Kaka niko bize kidogo nafanya interview na BBC Swahili nitakutafuta
baadae”.Nikasema poa kaka ila kuna kitu nataka tuongee.
Mwandishi akiwa hana hili wale lile siku ya jumatano asubuhi
saa 7:12 simu yake iliita kutazama jina
alikuwa ni Steve Yanga…….na maongezi yalikuwa hivi
Manjale:Nikiwa nimekariri Mambo vipi Steve Yanga?
Steve:Aah!!Manjale
hilo jina silitaki kama huwezi kuniita Steve Azam basi ishia Steve.Vipi
tunahitaji kuonana ana kwa ana ama hata kwa simu inatosha?
Manjale:Ikabidi niwe mpole pale nikamwomba msamaha rafiki
yangu huyu na michapo ikaendelea.
Steve:Manjale
vipi ni kipi hicho unachotaka kujua?afu ujue sifanyagi interview bure bure kaka
ila kwasababu ni wewe tuendelee.
Manjale:Eehe!!Kaka
vipi hili la wewe kuhamia Azam ni kweli?
Steve:Manjale
ulichokisikia na kukiona kwenye mitandao
ni kweli kabisa mimi kwa sasa siyo shabiki wa Yanga tena nguvu na akili yote
iko Azam Fc wazee wa mipango hai.
Manjale:Duh
makubwa!!Hebu kwanza rudi nyuma kidogo unipe historia yako fupi hasa ni lini
ulianza kuishabikia Yanga?
Steve:Kwa kusema
ukweli (msishangae huyu jamaa katokea Mbeya kwa kuchapia jina langu) Mwanjala
mimi nilianza kuishabikia Yanga mwaka 2008 na jina langu lilikuja kufahamika
sana baada ya kulia pale uwanja wa taifa siku Yanga ilipofungwa goli 5-0 na
Simba.Kabla ya hapo hakuna shabiki wa kiongozi wa Yanga aliyekuwa akinifahamu
lakini baada ya picha zangu na clip kusambaa kwenye matelevisheni na mitandao
mbalimbali ya kijamii nilianza kutwafutwa na kupongezwa kuwa mimi ni shabiki wa
ukweli kabisa.
Manjale:Aisee safi sana,Eeh vipi hebu tuambie nini kimekutoa
Yanga na kukupeleka Azam?
Steve:Manjale,baada ya mimi kutoka katika shindano la Kwetu House lililokuwa chini ya Azam
Media ambalo hata wewe Manjale ulikuwepo,maisha kwangu yakawa magumu.Watu wakaanza
kunisakama na kuniita msaliti eti kwanini nimeingia katika shindano hilo wakati
Azam na Yanga hawapatani?Nikawa sina raha huyu anasema hiki Yule ansema
kilebasi ikawa ni shida mtindo mmoja.Kwakweli nilikuwa naumia sana na kujiuliza
maswali mengi kwanini hivi…….kosa langu
ni lipi hapa?kwenda kwenye shindano hilo ndiyo iwe tabu?
Manjale:Aisee pole sana Steve….vipi ni sababu hiyo tu ama
kuna nyingine?
Steve:Sababu nyingine ni kwamba nimekuwa sina maelewano mazuri
na baadhi ya viongozi wa Yanga kwani wamekuwa wakinitolea lugha chafu pindi
ninapokuwa nikiwafuata kwa maswala mbalimbali mfano……. na …….(akawataja
viongozi hao).Lakini napenda sana kumshukuru Mwenyekiti Yusuph Manji kwa zawadi ya bodaboda na cheti.
Manjale:Hebu niambie Azam wanajua uwepo wako kama shabiki wao
na ilikuwaje?
Steve:Azam wanajua hilo na kabla sijafanya maamuzi hayo
niliupigia simu uongozi na kuongea nao kirefu.Nashukuru wamenielewa na
kunipokea kwa mikono wiwili.
Manjale:Safi kaka,nasikia wanataka kukupa ajira pia?
Mwandishi wa habari hii akiwa na waliokuwa washiriki wenzake aktika shindano la kwetu house |
Steve:Aah Manjale
umepata wapi habari hizo?Ila ni kweli hiyo ishu ipo japo haijawa rasmi sana
ikiwa tayari nitakwambia.
Manjale:Basi poa Steve asante sana kwa ushirikiano wako
Steve:Poa poa kaka panapo chochote tutafutane
Manjale:Poa kaka tuko pamoja
Huo ndiyo ukawa mwisho wa interview yetu,nadhani lile giza
tulilokuwa nalo juu ya uamuzi wa huyu shabiki limeondoka na kila kitu kiko
hadharani.
Asante kwa kuwa pamoja nasi……………….”karibu kwa
maoni yako”
0 comments:
Post a Comment