MAKALA YA LEO
Na. ALLEN
KAIJAGE aka middle ya juu
0655106767
kaijagejr@gmail.com
Ukitaka
kuona maajabu jaribu kuthubutu kutembelea Tanzania.Kuna vitu vya ajabu ambavyo
bila shaka vitakushangaza.Najua utafikiria kuhusu mlima Kilimanjaro na baadhi
ya hifadhi za taifa kama Serengeti,manyara na mikumi.Lakini milima mikubwa na mbuga za wanyama hazipatikani Tanzania pekee,kuna nchi nyingi zinamiliki
mbuga na milima mikubwa.Lakini kuna vitu vya pekee vinapatikana Tanzania tu na
hutothubutu kuvisikia nchi nyingine.
Achana na
madini ya tanzanite ambayo yanapatikana Tanzania pekee pia kuna aina ya watu
wanapatikana Tanzania tu.Ni Tanzania tu mtu mwenye shahada ya ualimu anafanya
kazi ya udaktari,mtu mwenye shahada ya sheria anafanya kazi ya usanifu majengo
na mtu mwenye shahada ya uhasibu anafanya kazi ya uhandisi.Alafu tunategemea
vitu bora kutoka kwa watu hao.Hiyo ndio Tanzania yangu.Kila sekta kuna watu
wajanja wajanja ambao wana maneno mazuri ya ushawishi lakini ni
wababaishaji.Kwenye sekta ya afya ndio hao wanaopasua watu vichwa badala ya
miguu,kwenye sekta ya ujenzi ndio hao wanaojenga ghorofa leo keshokutwa
linaanguka na kwenye michezo ndio hao wanaorudisha michezo yetu nyuma kwa
kufanya kazi ambazo aziwahusu kwa manufaa yao.
Huku kwenye michezo ndio kunaongoza kwa
makanjanja.Hawa wengi ni viongozi wajanja wajanja wanaofanya ujasiriamali
kwenye michezo yetu.Kiongozi amepewa dhamana ya kuwa katibu lakini anataka
kuingilia na kazi ya kocha,hapa unafikiri kocha atakuwa na sauti gani kama bosi
wake ameamua kuingilia kazi yake?.Je unafikiri kocha huyo atafanya kazi yake
kwa usahihi kama maamuzi ya kazi yake anafanyiwa na katibu wake?.Wana uchumi
wanaamini ili upate uzalishaji mkubwa lazima ufanye kitu kinaitwa Division of
labour(mgawanyo wa kazi) ila viongozi wa michezo yetu hususani mpira wa miguu hawataki
kufuata sheria hiyo ya wachumi kwa kulinda matumbo yao
Wakati
napata habari za kufukuzwa kwa kocha logarusic wala sikustushwa.Kwani hiyo ni
kawaida kwa timu zetu.Labda ningekua sio mtanzania hapo ndipo ningeshangaa kwa
kocha aliyeongezewa mkataba anafukuzwa kabla hata ligi kuanza.Sawa kocha
anaweza kuwa na matatizo lakini viongozi wa simba watakua na matatizo
zaidi.Kocha loga kabla ya kutimuliwa kuna mahitaji aliwasilisha kwa viongozi
kabla ya kuondoka lakini mahitaji yake hayakutimizwa.Kocha anahitaji kipa mrefu
analetewa kipa ambaye hamuhitaji unafikiri hapo kuna nini kama si ukanjanja wa
viongozi wa simba.
Tatizo la viongozi wetu hawa ni ujuha wao wa matatizo ya ufundi kuliko
kocha.Kila kiongozi akiona mchezaji anamvutia machoni mwake hulazimisha
kusajiliwa hata kama si chaguo la kocha.Nani kawaambia mpira wa kisasa
unaendeshwa hivo?. Mpira wa kisasa hauendeshwi kwa faida ya mtu binafsi.Tatizo la simba si kocha bali
ni viongozi.Makocha wangapi wanakuja na kuondoka?.Hao wakina phiri na milovan
ambao ni vipenzi vya mashabiki wa simba walishawai kuja na kuondoka zaidi ya
mara moja.Mashabiki wa simba kama mngepata nafasi ya kuwauliza sababu za
kuondoka kwa makocha hao vipenzi vyenu bila shaka wangewaambia ni viongozi
tu.Kwa simba wasipobadilisha mfumo wao wa madaraka hata aje sir alex ferguson
au arsene wenger watatimuliwa tu.Kocha inabidi apewe nafasi ya kutoa maamuzi
yote yahusiyanayo na mambo ya kiufundi.Kocha inabidi apewe nafasi ya kusajili
wachezaji anaowataka bila kusahau
kupanga wachezaji anaowataka kwenye mechi husika.Maamuzi ya kocha inabidi
yaheshimiwe na watu wote ikiwamo viongozi.Kocha mkishampa dhamana inabidi mumpe
uhuru wa kufanya kazi yake sambamba na kumtimizia mahitaji
yake ili pindi anapokosea muwe na nguvu ya kumhukumu.
Timu zetu
haziwezi kukaa na kocha hata miaka mitatu tu kwasababu ya matatizo ya viongozi
wetu.Kocha kama ferguson amekaa miaka mingi Manchester united kwasababu ya
viongozi bora aliowakuta ndani ya timu.ferguson angekua simba au yanga
angeshasahaulika zamani kwenye ramani ya soka lakini mpaka sasa ni mtu na
heshima zake kwenye jiji la Manchester.Viongozi walimpa kila kitu anachohitaji
pia wakamuamini na kumvumilia na mpaka sasa ukizungumza kuhusu manchester
united lazima umtaje sir alex.Ulishawai kujiuliza kama Manchester united
wangemtimua sir alex baada ndani ya miaka minne ya mwanzo ambayo alikaa bila
kombe lolote je Manchester united ingekuwa kama ilivyo sasa?.Kwangu mimi jibu
ni hapana ila sitaki kuishi ndani ya ubongo wako na kuhisi jibu lako.
Wapo
makocha wengine wengi waliokaa kwa muda zaidi ya miaka 10 kwenye timu zao kama
arsene wenger,sam allardyce na wengine wengi,Makocha hao wamekaa miaka mingi
kwenye vilabu vyao kutokana na uongozi imara wa vilabu husika.Lakini kwa
viongozi wetu wenye siasa nyingi na akili nyingi za kutunisha matumbo yao kupitia timu zetu
tutaendelea kufukuza makocha kila iitwapo leo.Muda mwingine huwa nawalaumu sana
hawa wanachama wa vilabu vyetu kwa kurudisha miaka nyuma.Kila siku wanawapa
dhamana watu wale wale na watu hao hufanya mambo yale yale ya kuendelea
kudumaza vilabu husika.Kwa msisitizo kabisa nawaambia wanachama hao matatizo
ndani ya timu zenu haziletwi na makocha bali viongozi wenu mnaowachagua kila
siku.Loga usihuzunike kufukuzwa,hii ndio Tanzania na maajabu yake hata ferguson
akija kufundisha vilabu vyetu watamtimua tu.
0 comments:
Post a Comment