Kutoka gazeti la Independent la leo jumapili
habari zinasema moja kati ya kipengere ambacho hakikuwa kimewekwa wazi na klabu
ya Manchester United juu ya usajili wa mshambuliaji hatari raia wa Colombia
Radamel Falcao Garcia Zarate ni kwamba United haitasita kumrudisha haraka nyota huyo katika klabu yake mama ya Monaco ikiwa tu ataumia tena goti
lake.
Falcao ambaye mapema
mwaka huu aliumia goti na kukaa nje kwa miezi sita (6) na kupelekea kuikosa
michuano ya kombe la dunia nchini Brazil inasemekana kuwa mbali ya gharama zake
za uhamisho wa mkopo kuwa juu pia kiwango cha mshahara alioukitaka ni sababu
nyingine iliyoifanya Manchester United kuweka masharti magumu katika mkataba wa
nyota huyo mwenye jicho la goli.
Hivyo basi uwepo wa
Falcao Manchester United mbali ya kutegemea sana kiwango kizuri kitakacho ambatana
na mvua ya magoli pia suala la afya ni jambo jingine kubwa litakalo mfanya nyota
huyo aendelee kubaki Old Traford na hatimaye kupata mkataba wa kudumu wakati wa
majira yajayo ya kiangazi.
Je,Falcao ataepuka jinamizi la majeruhi na kubaki Old Traford?ni jambo la kusubiri na kuona....
Je,Falcao ataepuka jinamizi la majeruhi na kubaki Old Traford?ni jambo la kusubiri na kuona....
0 comments:
Post a Comment