Habari na Paul Manjale
Nyota kinda wa klabu ya
Arsenal Mcosta Rica Joel Campbell ameshangazwa na uwezo wa nyota mwenzie katika
klabu hiyo Muhispania Santi Cazorla na kusema ajabu ajabu!!
Campbell akifanya
mahojiano na mtandao wa klabu hiyo uitwao Arsenal Player alisema “Cazorla
anashangaza sana,anafanya nijiulize mara mbilimbili yeye ni mchezaji wa aina
gani? nadhani ni aina ya peke yake”
“Lazima nikiri Cazorla
ni mchezaji wa aina yake.Anaweza kupiga kona ama faulo sawa sawa kwa miguu yote
bila kuonyesha tofauti yoyote ile.Anachokifanya kwa mguu wa kulia ndicho
anachokifanya kwa mguu wa kushoto.Hicho siyo kitu cha kawaida kukiona ananishangaza
kwakweli.”
Akiulizwa kuhusu
ushindani wa namba uliopo katika kikosi hicho hasa sehemu ya ushambuliaji Campbell alisema “ Nadhani kila mchezaji
atakuwa sambamba kugombea nafasi kikosi cha kwanza.Mshindani wangu mkubwa ni
mimi nahitaji kufanya bidii mazoezini kila siku ili niweze kuwa bora zaidi.Ni
heshima kuwa hapa leo”
“Nadhani ninaweza kuongeza kitu kikosini mfano
kasi,magoli hata uwezo wa kukokota mipira.Mimi ni mchezaji mwenye uwezo wa
kucheza kulia,kushoto ama kati kama mshambuliaji pekee”.
“Ni jukumu la mwalimu
kunipanga sehemu anayoona ninahitajika zaidi na nitajitahidi kufanya vizuri. ” Alimaliza
Campbell shujaa wa Costa Rica katika fainali zilizoisha za kombe la dunia
nchini Brazil.
0 comments:
Post a Comment