Vilabu vya jiji la London Chelsea
na Arsenal vimeingia katika vita kali ya kumtaka mlinda mlango kinda raia wa
Ubelgiji Mile Svilar (15) ambaye anafananishwa na mlinda mlango namba moja wa
klabu ya Chelsea Thibaut Courtois.
Inasemekana klabu ya Arsenal
tayari imeshampa kinda huyo mwaliko wa kutua Emirates kwa ajili ya
majaribio ya siku kadhaa.Klabu ya Chelsea yenyewe tayari imeripotiwa
kukamilisha zoezi hilo mapema.Wakati huohuo klabu ya Manchester United nayo imeripotiwa
kumuulizia kinda huyo.
Lakini baba mzazi wa kinda
huyo,Ratko Svilar ambaye ni mlinda mlango wa zamani wa klabu ya Antwerp amesema
ofa yoyote toka vilabu vya England haitasikilizwa kwa wakati huu na badala yake
itapuuzwa kutokana na kuwa tayari wana makubaliano na klabu ya Anderletch.
Amesema “Mile ameshafanya majaribio na Chelsea,Manchester United wameshaanza
kumuulizia.Kila mtu anamtaka,lakini tayari tuna makubaliano na Anderletch japo
hatoweza kusaini mkataba mpaka atakapofikisha miaka 16.Sidhani kama kuna sehemu nzuri kwake kwa sasa zaidi ya
Anderletch”
0 comments:
Post a Comment