Habari na Paul Manjale
Unamkumbuka yule winga
mrefu wa klabu ya Newcastle United,Yule aliyekuwa na nywele ndefu na
nzuri kama za akina Rihanna na Beyonce?Hapa namuongelea Jonas Gutierrez
Je,ukimuona leo utamtambua?unajua aliko,anachezea klabu gani kwa sasa?
Gutierrez anavyoonekana sasa |
Haya ni baadhi tu ya maswali ambayo
unaweza ukajiuliza kwa haraka haraka na usipate majibu ya uhakika juu ya nyota
huyu wa soka.Nani alimjua kabla ya kutua Newcastle misimu kadhaa nyuma,nani
anayejua aliko?Siyo maarufu sana kama akina Messi,Di Maria ama Aguero lakini
kwa sasa anaweza akawa na kitu ambacho mimi na wewe tungependa kukifahamu.
Gutierrez huyu wa sasa siyo Yule
tunayemfahamu,siyo Yule tuliyezoea kumuona kila wikendi akiwa na jezi za rangi ya punda milia
akisukuma gozi la ng’ombe pale katika dimba la St.James Park na madimba mengine
England.Gutierrez wa sasa ni mgonjwa,hawezi tena kufanya zile vurugu zake
uwanjani,hawezi tena kukimbia kwa ile kasi tuijuayo….Gutierrez anaumwa
Kansa.Soka ndiyo basi tena anaungana na nyota kama Jason Cundy (1997
aligundulika kuwa na kansa),Alan Stubbs (1999),John Hartson (2009) na Stiliyan
Petrov (2012).
Jonas Guttierrez amefichua kuwa mgongano
kati yake na aliyekuwa mlinzi wa kulia wa klabu ya Arsenal Mfaransa Bacary
Sagna ulifanya afanyiwe vipimo ambavyo ilikuja kugundulika kuwa nyota huyo ana
Kansa.
Nyota huyo wa zamani wa Newcastle
amekuwa akipambana na ugonjwa huo kwa mwaka mmoja sasa hata kupelekea
kuondolewa kwa korodani/kende yake ya kushoto mwezi Octoba mwaka jana.Gutierrez
ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 31 aliyasema hayo jumanne wiki hii wakati
akifanya mahojiano na chombo kimoja cha habari kiitwacho TYC Sports cha nyumbani kwao Argentina.
Alisema “Ilikuwa ni Mei 2013,niligongana
vibaya na Sagna nikaumia maeneo ya viungo vya uzazi.Tangu hapo nikawa na
maumivu makali mno ambayo hayakuisha.Niliongea na Daktari mara moja na
akaniambia usijali yatapoa tu.
Gutierrez akigugumia kwa maumivu baada ya kugongana na Sagna |
“Hali ilijirudia tena wakati wa
likizo na nikajisikia maumivu sana
sehemu ya korodani.Kuna wakati korodani zilichachamaa mpaka nikawa nashindwa
kuvaa nguo za ndani.Nilirudi kwa daktari
na kumsimulia kila kitu,akanishauri nifanye vipimo vya Ultrasound ambayo
vilikuja kugundua kuwa nina uvimbe/mtutuko na nilipaswa kufanyiwa upasuaji
mapema”
Baada ya kuambiwa nijiandae kwa
upasuaji niliondoka nikilia na kurejea nyumbani na kumwambia yote baba yangu aliyekuwa
amekuja kunitembelea.Niliongea na uongozi wa klabu juu ya tatizo langu na nia
yangu ya kutaka kwenda kutibiwa nyumbani Argentina, nikaruhusiwa.
Gutierrez alirudi England katika
klabu yake ya Newcaste baada ya upasuaji na kukutana na balaa toka kwa kocha wake
Alan Pardew….anasema
“Niliporejea kikosini mwishoni mwa Novemba kuendelea na
utaratibu wa mazoezi,timu ilikuwa vizuri lakini katikati ya mwezi wa Desemba
kocha Pardew aliniambia huna nafasi tena kikosini na badala yake tafuta timu
ukacheze kwa mkopo.Nilishangazwa sana na uamuzi ule ukizingatia nimekuwa nikicheza
karibu kila siku kwa kipindi chote cha miaka mitano ambacho nimekuwa hapa,sasa
iweje wanitoe kwa mkopo?iliniuma sana.Sikuwa na jinsi nikaenda Norwich City kwa
mkopo mwezi januari.
Je,vipi bado una
mkataba na Newcastle na vipi kuhusu gharama za matibabu unalipia wewe au wao?
Gutierrezi “Ndiyo bado nina mkataba
nao ambao unaisha msimu huu,najilipia mwenyewe matibabu,pesa siyo kitu muhimu
zaidi.Kitu muhimu ni uzima.
Huna korodani/kende
moja je vipi wazazi wakihitaji wajukuu?
Gutierrezi “Unapokuwa na tatizo kama
hili wanakupeleka kwenye benki ya kuhifadhia mbegu za kiume na unaacha sample
kadhaa za mbegu hapo kama tahadhari ikiwa kende nyingine itaharibika.Lakini
naamini kwamba nyingine iko vizuri hakuna kitakacho haribika”
Sasa kwanini umechelewa
kuupasha habari umma kuhusu ugonjwa wako na hata useme sasa?
Gutierrezi “Ni jambo binafsi sana
lakini juzi nilipata email(barua pepe) kuhusu mwigizaji mmoja wa kike ambaye
nae ana pambana na tatizo kama langu na alikuwa akionyesha picha zake hadharani
za wakati akiwa na nywele zake na alipoanza kupoteza nywele na yote aliyokuwa
akiyapitia.Nikaona na mimi napaswa kusema ili watu wajue na labda inaweza kuwa
ni msaada kwa wengine”
0 comments:
Post a Comment