Timu ya taifa ya Brazil imepata ushindi wake wa kwanza
tangu kuondolewa kwa aibu ya kubugizwa
goli 7-0 na Ujerumani katika mchezo wa
nusu fainali wa kombe la dunia zilizofanyika nchini kwao miezi miwili iliyopita
baada ya alfajiri ya leo kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Colombia katika
mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Neymar akishangilia goli dhidi ya Colombia |
Huu unakuwa ni mchezo wa pili kwa miamba hiyo kukutana ikiwa
imepita miezi miwili na siku kadhaa tangu timu ya taifa ya Brazil ilipofanikiwa
kuwafunga na kuitoa Colombia kwa goli 2-1 katika mchezo wa robo wa kombe la
dunia uliopigwa katika dimba la Fortaleza ambayo nyota wa Brazil Neymar
alichezewa rafu iliyopelekea nyota huyo kuvunjika mfupa wa mgongo.
Neymar akiwania mpira na mlinzi wa Colombia Zuniga |
Brazil iliyokuwa chini ya kocha mpya Carlos Dunga na nahodha
mpya Neymar Dos Santos ilijipatia goli lake la ushindi na la pekee kupitia
Neymar dakika ya 83 kwa mkwaju wa adhabu
uliomshinda mlinda mlango David Ospina na kuamsha ndelemo hoi hoi na vifijo
kutoka wa mashabiki wa timu hiyo waliojitokeza kwenye uwanja wa Sun Life,Miami
(Marekani) uliokuwa na jumla ya watazamaji 73,429.
Falcao akigombea mpira na walinzi wa Brazil Luiz na Maicon |
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Dave Gantar
ilishudiwa mwamuzi huyo akipata wakati mgumu kutokana wachezaji wa timu zote
mbili kuchezeana rafu mara kwa mara kulikopelekea kutolewa kwa jumla ya kadi saba za njano
kutolewa huku winga wa Colombia Juan Quadrado akitolewa uwanjani baada ya
kuonyeshwa kadi mbili za njano kufuatia kumchezea rafu Neymar katika matukio mawili tofauti.
Cuadrado na Felipe Luiz wakigombea mpira |
Huu unakuwa ni mchezo wa 61 wa kocha Dunga akipata ushindi
katika michezo 43 akitoka sare 12 na
kufungwa 6 pekee ndani awamu mbili
alizofundisha akiwa kama kocha mkuu wa timu hiyo.Dunga ambaye amerithi mikoba
ya kocha aliyetimuliwa Felipe Scolari aliita wachezaji kumi tu waliokuwepo
katika fainali za dunia huku wanne pekee wakianza katika kikosi chake cha kwanza.
0 comments:
Post a Comment