Habari na Paul Manjale
Mshambuliaji
na nahodha wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England Wayne
Rooney amemfananisha winga kinda wa nchi hiyo Raheem Sterling na winga nguri wa
zamani wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Uhoranzi Marc Overmars.
Rooney
akifanya mahojiano kabla ya mchezo wa leo wa kusaka tiketi ya kushiriki
michuano ijayo ya Ulaya (Euro 2016) dhidi
ya timu ya taifa ya Uswisi.
Alisema “Nilikaa nae chini kabla ya kombe la dunia nikamwonyesha video za Marc Overmars
kwasababu ananikumbusha mno vitu vya mkongwe yule”
“Nafikiri
ana uwezo wa kuwa bora zaidi kama alivyokuwa Overmars.Bado ni mdongo lakini
uwezo anaounyesha ni wa ajabu sana”.
“Ni
mchezaji mzuri sana.Hili lilijionyesha msimu uliopita na hata mwanzo wa msimu
huu”
“Ni
mchezaji mzuri anaweza kucheza mbele kabisa
ama pembeni.Japo ana umbile dogo lakini ni mjanja, imara na ana nguvu
sana”
“Atakuwa
ni mchezaji muhimu sana kwa kipindi cha miaka 10 au 15 kwa England na na bahati
mbaya kwa klabu yake ya Liverpool”.Alimaliza Rooney ambaye leo atakuwa na
kibarua kigumu cha kukiongoza kikosi cha England kupata pointi tatu muhimu
mbele ya wenyeji Uswisi.
0 comments:
Post a Comment