MAKALA YA LEO
Allen kaijage
0655106767
kaijagejr@gmail.com
Azimio la
Arusha si neno geni kwa Watanzania.Wengi wao tumelisikia kama hatukusoma
sehemu,Pia wachache kati yetu walikuwepo kipindi cha azimio la Arusha.Azimio la
Arusha ni tamko rasmi la kisiasa lililokusudiwa kuingoza nchi yetu katika
misingi ya ujamaa.Azimio hili lilipitishwa jijini Arusha chini ya uongozi wa
baba wa taifa hayati mwalimu Julius K.Nyerere mnamo mwaka 1967. Lengo kuu la
azimio la Arusha ilikua ni kupunguza au kuondoa unyonyaji na uonevu wa
mabepari.Kwa hekima za mwalimu nyerere akaona sera ya ujamaa na kujitegemea ndo
utakuwa mwarobaini kwa mabeberu na kuleta ustawi ndani ya nchi.
Uzalishaji ulipungua kwa kiasi kikubwa uliopelekea wananchi kuikatia tamaa sera ya ujamaa.Labda ni kwasababu ya Vita ya Uganda au anguko la bei ya bidhaa zetu ama tatizo la kimataifa la mafuta miaka ya mwanzoni mwa 1970.Hizo zote zinaweza kuwa sababu ya kufeli kwa ujamaa.Mwalimu kwa busara zake ilipofika mwaka 1985 akatangaza kutogombea tena urais na kumwachia rais mwinyi aliyeingia nchini na taratibu za soko huria na huo ndio ukawa mwanzo wa kufa kwa ujamaa.
Soko huria
(Open market )ndio mfumo unaoendesha
dunia ya sasa.Soko huria imefungua milango kwa wafanyabiashara kuuza au kununua
bidhaa kokote wapatapo soko.Wana uchumi wanasema kuwa katika dunia ya sasa
hakuna nchi ambayo ni wajamaa tu(pure socialist) wala mabepari tu(pure
capitalist) zaidi ya nchi nyingi kuchanganganya ubepari na ujamaa(mixed
economy).Huku misingi ya ubepari ikilenga ushindani wa kibiashara wakati ujamaa
ukilinda utu.Hapo utaona Dunia kwa ujumla imeruhusu ushindani huru wa
kibiashara kwa misingi isiyo ya unyonyaji.Utapata zaidi ya
utakavyozalisha.Utapata kiasi cha jasho lako huku lazima ukubali kuliwa ili
ule.
Sera hii inatawala sekta zote duniani.Hata
sekta ya michezo pia inahitaji uwekezaji wa hali ya juu kufikia mafanikio.Ndio
maana nchi zilizofanikiwa sana kwenye michezo hasa soka ni zile zilizowekeza
zaidi kwenye mchezo huo.Hata vilabu vilivyofanikiwa Duniani ni vile
vilivyowekeza zaidi kwa wachezaji.Lakini bado kuna watu wabishi wanaoamini
ujamaa katika soka .Wapo macommunist
wanaofikiri watafanikiwa kwa sera zao za kale.Wapo macomunist wengi lakini leo
ntamzungumzia mmoja.
maswahiba mazito kutoka kwa Chelsea,City na Liverpool lakini
bado wenger ni Yule Yule asiyetaka kujifunza kutoka kwenye majanga yaliyomsibu.
Ukiangalia
kikosi cha Arsenal utaona mapungufu kwenye nafasi ya ushambuliaji bila kusahau
nafasi ya kiungo mkabaji.Lakini wenger bado amefumbia macho swala hili na
kuendeleza sera zake za ujamaa akiamini ujio wa welbeck akisaidiana na sanogo
watafunga magoli mengi huku akisahau mabepari City wana Aguero,Dzeko na
Djovetic ,Chelsea wana Costa,Drogba n a
Remmy.Huku mabepari hayo yakiwa na viungo wakabaji wa nguvu kama Fernandinho na
Fernando kwa upande wa city,Matic na mikel kwa upande wa Chelsea yeye mcomunist
ana wazee arteta na flamin ambao wote
damu zimeshachoka.
Hapo mjamaa wenger kila siku
ataendelea kulalamika kuhusu vitendo vya unyanyasaji na
uonevu anavyofanyiwa mabepari wa City na Chelsea ilihali ana uwezo wa
kubadilisha mawazo yake ya ujamaa na kuingia moja kwa moja kwenye Dunia ya
ushindani kuwakabili mabeberu hayo.Wenger amejua kuiga mfumo wa uchezaji wa
Barcelona ila ameshindwa kugundua Barcelona pia wameachana na sera ya ujamaa na
kuingia kwenye mixed economy (kuchanganya ubepari na ujamaa) ndio maana utaona
Barcelona ya sasa inatumia bajeti ya usajili wa wachezaji wote wa arsenal
kumnunua luis suarez na kuacha utamaduni
wao wa kuwaamini wakina Tello na Bojan.
Dawa ya
moto ni moto.Dawa ya bepari ni bepari na beberu ni beberu.Wenger kama anataka
kuondoa aibu ya vipigo vya magoli mengi anavyovipata kutoka kwa city na Chelsea
na kukabiliana nao jino kwa jino inabidi aachane na misingi ya azimio la Arusha
na kuvaa roho ya ubeberu.Asikwambie mtu Arsenal haiwezi kushindana na City na
Chelsea,Arsenal ni timu tajiri kuliko City na Chelsea tofauti yao inakuja
kwenye sera ya usajili ya klabu.
0 comments:
Post a Comment