Baada
ya kuwa nje kwa kipindi kirefu kutokana na majeraha ya mara kwa mara hatimaye
kiungo Abou Diaby anarejea leo dimbani kuichezea klabu yake ya Arsenal katika
mchezo wa kombe la Capital One dhidi ya klabu ngumu ya Southampton.Diaby amekuwa
nje ya dimba kwa kipindi cha siku 556 tangu alipoumia Machi 2013 katika mchezo
dhidi ya Swansea.
Akielezea
kurejea huko kwa kiungo wake kocha Arsene Wenger amesema “Diaby alicheza dakika
90 wiki iliyopita katika mchezo uliovikutanisha vikosi Arsenal na Aston Villa
vya wachezaji waliochini ya miaka 21 (U21) hivyo atakuwepo katika mchezo wa
jumanne dhidi ya Southampton”.
“Yuko
vizuri kiafya na kiakili mara zote amekuwa akirejea dimbani licha ya kukumbwa
na majeraha,ni mtu anayejitolea kwa ajili ya timu hivyo mchango wake unahitaji
kuheshimiwa.Mimi ni muumini mkubwa wa soka yake lakini nasikitika kwakuwa
ameshindwa kuionyesha kutokana na kuumia umia”
Mbali
ya Diaby pia kocha Wenger amepanga kuwapa nafasi makinda na wachezaji wanaokosa
namba kikosi cha kwanza katika mchezo huo huku akiwaapumzisha wachezaji wake
wengi wazoefu kwa ajili ya mchezo wa wikendi hii dhidi ya mahasimu wao
Tottenham hotspurs.Baadhi ya makinda watakaocheza leo ni Hector Bellerin,Isack
Hyden,Chuba Akpom,Semi Ajayi watakaosaidiana na wazoefu Joel Campbell,David
Ospina pamoja na Lukas Podolski.
Michezo
mingine ya Capital One ikiwa ni roundi ya tatu ni kama ifuatavyo
Liverpool
vs Middlesbrough
Swansea
vs Everton
Sunderland
vs Stoke
Mk
Dons vs Bradford
Kesho
jumatano ni tarehe 24
Chelsea
vs Bolton
Crystal
palace vs Newcastle
Man
City vs Sheff Wed
West
Brom vs Hull
0 comments:
Post a Comment