Klabu ya Chelsea
huenda ikauhama kwa muda uwanja wake wa Stamford Blidge maarufu kama
darajani na kuhamia uwanja wa Twickenham.Habari za kuaminika zinasema klabu
hiyo iko katika mazungumzo mazito ya kuomba kuutumia uwanja huo kwa msimu mmoja
wa 2016/17,Twickenham ni uwanja maarufu sana kwa mchezo wa rugby jijini London
na haujawahi kutumiwa kwa soka tangu kujengwa kwake.
Twickenham kwa nje |
Ikiwa ombi hilo litafanikiwa Chelsea itautumia uwanjao huo
kwa mechi zake za nyumbani na hivyo kutoa nafasi kwa uwanja wa Stamford Blidge
kufanyiwa upanuzi toka idadi ya sasa ya watazamaji 41,800 mpaka 60,000 na hivyo
kuifanya miamba hiyo kuwa na msuli wa kuchuana kiuchumi na vilabu vingine
vikubwa Ulaya kama Manchester United,Arsenal,Bayern Munich,Barcelona na Real
Madrid.
Kwa ndani |
Hili litakuwa ni jaribio la pili la mmiliki wa klabu ya
Chelsea kuwa na mipango kama hiyo baada ya mara ya kwanza kufanya mipango
iliyokuja kushindikana ya kuhamia Battersea Power Station kusini mashariki mwa
London.
NB;Stamford Blidge ulianza kutumiaka mwaka 1876 mpaka sasa
umeshafanyiwa upanuzi mara mbili na ni uwanja wa nane (8) kwa ukubwa kati ya
viwanja vinavyotumiwa kwa mechi za ligi kuu.
Wakati huo huo kampuni ya Kituruki ya safari za anga ya Turkish Airline
imetangaza kupitia mtandao wake kuwa imefikia makubaliano ya kuidhamini klabu
ya Chelsea.Nembo ya Turkish Airline itaanza kuonekana katika jezi na bidhaa
nyingine za klabu hiyo msimu ujao (2015-2016) na kuhitimisha safari ndefu
iliyokuwa na mafanikio na kampuni ya Samsung toka mwaka 2005-2015.
0 comments:
Post a Comment